KUOKOLEWA KWA NEEMA Na Askofu Mkuu Zakaria Kakobe. Watu wanaosema kwamba haiwezekani kuokoka duniani, wanasema hivyo, kwa sababu hawajui kwamba tunaokolewa kwa neem a tu! Biblia inasema katika WAEFESO 2:8-9, “kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu (yaani zawadi kutoka kwa Mungu); wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”. Tunasoma pia katika YOHANA 1:16, “Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema”. Iko siri kubwa iliyofichika katika maana ya neno, “Neema”.Kama sisi sote tungefahamu jinsi tunavyookolewa kwa neema, na jinsi tunavyopokea neema juu ya neema; kwa hakika, hakuna mtu hata mmoja ambaye angekwenda kwenye mateso ya moto wa milele. Wote tungekwenda mbinguni kirahisi sana, kwa kuwa tunaingia mbinguni, kwa neema tu; na Shetani asingepata mtu wa kukaa naye motoni, ila malaika zake tu, maana moto wa milele haukutengenezwa kwa ajili ya wanad...
Comments
Post a Comment