maombi na aina zake.
Maombi yenye nguvu Maana ya Maombi: Maana ya maombi ni kusema na Mungu au kuhitaji msaada toka kwa Mungu. Isaya 43:26, Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. Unikumbushe – Mungu anaposema tumkumbushe hana maana kuwa amesahau. Hapana. Ila anataka kuona moyoni umeweka nini. Ndiyo maana aliwaambia wana wa Israel kuwa “Niliwazungusha makusudi ili nione mioyoni mwenu mna nini.” Ndiyo maana tunatakiwa kuliweka Neno la Bwana mioyoni mwetu. Zab 119:10 Tuhojiane – Ni jambo la kumshukuru Mungu anayetupatia nafasi ya kueleza mambo yetu, kero zetu na shida zetu kwake kwa kuhojiana naye ili tupate kupewa haki zetu. Haki zetu: Katika Biblia ziko haki zetu nyingi sana ambazo Mungu wetu ametuahidi. Lakini bahati mbaya nyingi hatuzijuwi. Inatubidi kusoma Biblia kwa bidii ili Neno lake Kristo likae kwa wingi ndani yetu. Biblia ina mistari 31,173. Hebu jipime uone, wewe unaijua mingapi? Dan 9:1 – Daniel katika wakati wake alisoma kitabu alichokuwa ameandika n...


Comments
Post a Comment