URENO YAFUZU KOMBE LA DUNIA

URENO YAFUZU KOMBE LA DUNIA

Hatimaye Ureno imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Uswisi na kufanikiwa kukata tiketi ya moja kwa moja kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Mchezo huo wa kundi B umepigwa usiku huu ambapo mabao ya Ureno yamefungwa na Djourou (bao la kujifunga) pamoja na Silva na sasa Uswisi iliyoishia nafasi ya pili ikiwa na point sawa na Ureno, inaingia hatua ya mtoano.

Wakati Ureno wakishangilia, Uholanzi wameshindwa kufuzu kwa fainali hizo licha ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Sweden ambao wameingia hatua ya mtoano.

Uholanzi walihitaji ushindi wa angalau bao 7-0 ili wapitie hatua ya mtoano, lakini zoezi hilo limekuwa gumu kwa upande na hivyo kuwaachia Sweden ambao wanalingana point wote wakiwa na point 19 katika kundi A.

Katika kundi hilo la A, Ufaransa ambao tayari walishafuzu moja kwa moja, wamehitimisha kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Belarus mabao yakifungwa na Giroud pamoja na Griezmann.

Katika kundi H, Ugiriki imefanikiwa kuingia hatua ya mtoano baada ya kuifunga Giblaltar mabao 4-0, wakati Ubelgiji ambayo ilishafuzu ikipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya  Cyprus.

Comments

Popular posts from this blog

maombi na aina zake.

KUOKOLEWA KWA NEEMA